Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanachama wa UVCCM wa vyuo vikuu mkoani Tabora waliomtembelea Ikulu ndogo mkoani humo usiku wa kuamkia leo. Pamoja na mambo mengine Rais Kikwete aliwataka vijana hao kuzingatia masomo kwa nguvu zao zote, akisisitiza kwamba elimu ni ufunguo wa maisha hivyo wasome kwa bidii ili nchi ipate wasomi waliobobea katika kila nyanja katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe, Fatma Abubakar Mwassa (mwenye kitenge, kati) na Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini Mhe Suleiman Kumchaya (kulia) wakipozi na viongozi wa wanafunzi wa UVCCM vyuoni
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na viongozi wa UVCCM wa vyuoni Tabora
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa jumuiya hiyo vyuoni Tabora
Juu na chini Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wana UVCCM vyuoni Tabora
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na makada hao wa UVCCCM.