Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose akizungumza na wafanyakazi wakati wa Futari.JPG
Mkurugenzi wa Zantel, Pratpa Ghose akiongozana na Afisa Rasirimali watu, Francis Kiaga.
Wafanyakazi wa Zantel wakichukua chakula.
Wafanyakazi wa Zantel wakijumuika kupata futari.
---
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel jana iliwaandalia wafanyakazi wake futari katika makao makuu ya kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya wafanyakazi katika msimu huu wa mfungo wa Ramadhan.
Akizungumza na wafanyakazi hao wakati wa hafla hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Bwana Pratap Ghose aliwataka wafanyakazi hao kuimarisha urafiki na upendo kati yao.
Alisema kuwa katika kipindi hiki cha mfungo wafanyakazi wakiwa kama waumini wengine wa dini ni vema wakatambua kuwa kipindi hiki cha mfungo ni kipindi cha kukaa pamoja na kutafakari mazuri ambayo wanatakiwa kuyafanya kati yao pamoja na jamii nzima inayowazunguka.
“Hiki ni kipindi muhimu sana kwetu wafanyakazi wote kwa ujumla katika kujitafakari kwa kiasi gani tumeishi katika jamii zetu na wenyewe kwa ujumla huku tukijiimarisha zaidi katika imani zetu za kidini” alisema Pratap.
Katika hafla hiyo wafanyakazi hao walipata wasaha wa kuulizana maswali yahusuyo utendaji wa kazi zao pamoja na maswali mengine ya chemsha bongo.