Leo majira ya saa 2 asubuhi eneo la Kamata jijini Dar es Salaam imetokea ajali iliyoyashirikisha magari yapatayo matatu. Ajali hiyo watu wote wametoka salama bila hata mchubuko ukiacha mshtuko. Gari moja ndiyo iliyoumia sana. Mazingira ya ajali ni breki ya ghafla iliyomfanya dereva mwenye gari iliyoumia sana kukwepea upande wa kulia akakutana na gari aina pick up ambayo ndiyo iliyomgonga baada ya jitihada kubwa za kumkwepa.
Dada huyo alikuwa anawahi kazini ila hiyo pick-up ilifunga breki ya ghafla kwa vile mbele yake kuna gari ilisimama pia. Huyo wa nyuma alishtukizwa akashindwa kusimama ndio maana akakwepea kulia. Shukrani mdau wa Kajunason Blog.