Mratibu wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013, Abdallah Mrisho 'Abby Cool' (katikati), akiongea na wanahabari leo kuhusu burudani zitakazokuwepo siku hiyo.
Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangala (katikati), akielezea jinsi timu yake ya Simba (wabunge) watakavyoigaragaza Yanga katika mechi yao.
Mbunge wa Igalula, Dkt. Athumani R. Mfutakamba (wa kwanza kushoto), akiwawakilisha wabunge wa Yanga katika mkutano huo.
Mwanamuziki 'Diamond Platnumz' akieleza jinsi atakavyomfunika msanii Prezzo kutoka Kenya.
Afisa Masoko kutoka kampuni ya simu za mkononi Tigo ambao ni mmoja wa wadhamini wa Tamasha hilo, Alex Msigala akiongea na wanahabari jinsi kampuni yake ilivyojipanga kufanikisha Usiku wa Matumaini 2013.
Meneja Uhamasishaji Rasilimali kutoka TEA, Doreen Shekibula (katikati), akipongeza waandaaji wa Tamasha hilo.
Msanii Ray Kigosi (katikati) akijinadi kuwa atamvunja taya Mhe. Zitto Kabwe siku hiyo.
Mwakilishi wa Bongo Fleva, H-Baba akielezea jinsi timu yake itakavyotoa kichapo kwa wapinzani wao wa Bongo Muvi.
Jacqueline Wolper (katikati) akimtumia salamu Mhe. Halima Mdee kuhusu kichapo atakachomshushia siku hiyo.
...Akionyesha jinsi alivyojipanga kumchapa Mdee.
Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan akielezea alivyo fiti kumkabili JB.
Bondia Thomas Mashali akitoa tambo zake kuwa atampa kichapo Patrick Amote kutoka Kenya.
Bondia Francis Miyeyusho akiwaeleza wanahabari alivyo tayari kumkabili bondia Shadrack Muchanje kutoka Kenya.
Meneja wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti akiongea na wanahabari (hawapo pichani) jinsi bendi yake itakavyowafunika wapinzani wao Sikinde.
Kiongozi wa Bendi ya Sikinde, Habib Abbas 'Jeffa' naye akielezea jinsi bendi yake itakavyofanya makamuzi siku hiyo.
Sehemu ya wanahabari waliohudhuria mkutano huo.
Diamond Platnumz (kushoto) akiwa katika pozi na H-Baba baada ya mkutano huo.
---
Baadhi ya wasanii, wabunge na wanamasumbwi watakaoshiriki katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013, leo walikusanyika katika mkutano wao na wanahabari uliofanyika katika Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza jijini Dar na kuelezea jinsi walivyojipanga kuelekea katika tamasha hilo kubwa ambalo litafanyika Julai 7, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika tamasha hilo, wabunge wa Simba na wale wa Yanga watashuka dimbani kucheza soka huku baadhi yao wakishiriki katika mapambano ya ndondi dhidi ya waigizaji. Kwenye eneo la ndondi, Mhe. Halima Mdee atapigana na Jacqueline Wolper, Mhe. Zitto Kabwe na Vincent Kigosi ‘Ray’, Mhe. Ester Bulaya atavaana na Aunt Ezekiel huku balaa zaidi likitarajia kuandikwa na mabondia Patrick Amote (Mkenya) atakayevaana na Thomas Mashali (Mtanzania) huku Mkenya Shadrack Muchanje akipigana na Francis Miyeyusho (Mtanzania).
Burudani nyingine zitakazokuwepo siku hiyo ni wakali wa muziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Prezzo, ambao watashindana katika jukwaa moja ili kutafuta nani mkali zaidi.
Bendi za Msondo Ngoma, Mlimani Park ‘Sikinde’ na Jahazi zitawaburudisha mashabiki wao. Vilevile, burudani nyingine itatoka kwa wakali wa Temeke, Wanaume Family na Halisi, wataokata mapanga Taifa kwa staili zao za kuvutia.
Soka la kukata na shoka kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva litahakikisha linawapa raha mashabiki wa wasanii watakaoingia uwanjani siku hiyo
(PICHA ZOTE: RICHARD BUKOS NA DENIS MTIMA / GPL)