Wananchi wa Tanzania wameelezwa kuwa kazi ya kuboresha huduma za afya na afya ya mazingira na maji ni ngumu na kuwa inahitaji nguvu za pamoja kati ya jamii, halimashauri na wadau mbalimbali ili kupata mafanikio yaliyokusudiwa hasa ya uzuiaji wa magonjwa.
Akitoa nasaha wakati wa kufunga wa zoezi la utoaji wa huduma za afya kwa uwiano katika jamii kata ya Gombo la Mboto, Mgeni rasmi Mh. Jerry Silaa, Mstahiki Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala amesema huduma za afya na afya ya mazingira ni muhimu katika maisha ya kila siku ya binadamu.
Ameongeza kwa kuwapongeza sana wakazi wa Gomngo la mboto Markaz pamoja na viongozi wao kwa juhudi kubwa walioifanya katika kuhakikisha uwepo wa kituo cha tiba karibu na jamii na kuwa wanastahili kuwa mfano wa kuigwa na jamii zingine.
Aidha amesema hilo ni moja wapo katika utekelezaji wa agizo la Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika lengo lake la kupeleka huduma za tiba zikiwamo zile za zinazohitaji madaktari bingwa karibu na wananchi.
Pichani juu na chini ni wakazi wa Gongo la Mboto wakimsikiliza Diwani wao ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wakati wa kufunga zoezi la utoaji wa Huduma za Afya kwa Uwiano katika Jamii kata ya Gongo la Mboto.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dr. Asha Mahita akielezea dhamira ya Idara katika kuendeleza Afya ya Jamii kwa kusogeza Huduma za Afya karibu na Jamii, Huduma hizo zinahusisha matibabu kwa magonjwa mbalimbali kama Magonjwa ya Moyo, Kisukari, Malaria, Macho, Meno, Afya ya Akili, Ushauri na kupima VVU kwa hiari, Elimu juu ya Uzazi wa Mpango na Afya ya Uzazi, Afya ya Mazingira, Lishe, na Jinsia, pia ametoa tathmini ya wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto Markaz waliopatiwa huduma za Afya bure kwa zoezi lililofanyika kwa muda wa siku tatu ikiwemo Afya ya Akili, Kifua Kikuu na matibabu ya Ujumla.
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akifurahia jambo na mmoja wa wakazi wa kata ya Gongo la Mboto aliyefika katika Zahanati hiyo kupatiwa Huduma ya Bure.
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akipima Presha wakati wa kufunga zoezi la Utoaji wa Huduma za Afya kwa Uwiano katika jamii ikiwa ni ishara ya kuhamasisha watu kujenga utamaduni wa kupima Afya zao.
Wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto wakipatiwa dawa za bure baada ya kufanyiwa vipimo wakati wa kutoa Huduma ya Upimaji Afya Bure kwa wakazi wa kata hiyo iliendehshwa kwa siku tatu.
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akifurahi jambo na watoto waliofika katika Zahanati hiyo kupatiwa huduma ya Upimaji Afya bure.
Mtaalamu wa Magonjwa ya Kisukari kutoka Kituo cha Afya Amana Dkt. Abushiri Rajabu akitoa maelezo kwa Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa kuhusu Elimu anayotoa kwa jamii kuhusiana na Ugonjwa huo.