Aliyekuwa Mklurugenzi wa Wilaya ya Kilolo Mohamed Ngwalima (kulia), akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Geradi Guninita katika uzinduzi wa mradi wa ufugaji kukuKATIKA hali isiyo ya kawaida, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Mohamed Ngwalima amekutwa amekufa akiwa katika kochi la nyumbani kwake.
Hata hivyo ilielezwa kuwa kifo hicho cha Ngwalima kimezua maswali mengi kutoka kwa wananchi ambapo inadawa kuwa siku moja kabla ya kufikwa na mauti alikuwa safarini jijini Dar es Salaam
Akizungumzia kifo cha Mkurugenzi huyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Joseph Muhumba, alisema kuwa taarifa za kifo hicho alizipata muda mfupi baada ya kuachana naye wakitoa jijini Dar es Salaama katika kikao cha wadau wa zao la Chai.
“Tulikuwa wote Dar es salaam ambako tulikwenda kufuatilia masuala ya kiwanda chetu cha Chai, ambapo DED wangu Ngwalima alikuwa ni mzima. Baada ya kumaliza harakati hizo tukaingia wote katika kikao cha wadau wa zao la Chai nami niwa naelekea mkoani Dodoma.
“Na jana (juzi) asubuhi niliwasiliana naye nikiwa safarini kuja Kilolo akiniambia naye yupo Kibaha njiani kuja katika kituo chake cha kazi.
“Sikuapata taarifa za kuugua kwake lakini nami ndio nasikia kuwa amefariki Ngwalima hakuumwa kwani taarifa hizi zimetushtua sana watumishi na hata wananchi wa Wilaya ya Kilolo,” alisema Muhumba.
Hata Muhumba alisema siku moja akiwa na DED huyo alimueleza kuwa anasumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kisukari.