Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

ZANTEL YAZINDUA HUDUMA YA DAKTARI KWENYE SIMU YA MKONONI

$
0
0
Mmoja wa madaktari watakaoshiriki huduma ya 'Daktari kwenye simu yako ya Zantel', Dkt. Aidan Tumaini from Agha Khan kutoka hospitali ya Agha Khan akielezea namna huduma hiyo itakavyofanya kazi. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa BR Solutions, Bwana Richard Njau, akifuatiwa na Mkuu wa kitengo cha Rasirimali watu cha Zantel, Francis Kiaga, na Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
---
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imezindua ushirikiano na kampuni ya BR Solutions pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma ya ‘Daktari kwenye Simu yako’ ikiwa ni suluhisho la haraka na kiunganishi kwa wateja wa Zantel kuweza kuzungumza na daktari wakati wowote na mahala popote.

Huduma ya ‘Daktari kwenye Simu yako’ inawapa wateja wa Zantel fursa ya kupiga simu na kuongea na daktari, jambo ambalo litawasaidia kuokoa muda na fedha, lakini pia kupunguza usumbufu kwa wale wenye matatizo ya ghafla ya kuonanana na daktari.

Akizungumzia huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali watu cha Zantel, Francis Kiaga anasema, ‘Daktari kwenye simu yako’ inaonyesha namna kampuni ya Zantel ilivyo msitari wa mbele katika kuboresha maisha ya wateja wao kwa teknolojia ya simu za mikononi.

‘Kampuni ya Zantel imewekeza vya kutosha kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma ambazo zinaboresha maisha yao kupitia mtandao huu’ alisema Kiaga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya BR Solutions, Francis Njau alisema huduma hiyo imekuja kwa wakati muafaka na ni muhimu sana kwa watanzania wengi wanaohitaji ushauri wa daktari katika nyakati tofauti au kwenye matatizo ya ghafla.

“Huduma hii ni ya haraka, na unaweza kuipata wakati wowote, lakini pia itasaidia kupunguza gharama za kwenda kumuona daktari, au kwa wale wanaopata matatizo mida ya usiku itasaidia kupunguza usumbufu’ alisema Bwana Njau.

Huduma hii ya ‘Daktari kwenye simu yako’ itashughulika na magonjwa kama Ukimwi, cancer, Ugonjwa wa moyo, Malaria, Afya ya uzazi pamoja na huduma ya kwanza.

Kampuni ya Zantel imeshawahi kushinda tuzo za ubunifu katika kutumia teknolojia katika kuboresha afya na huduma yake ya Mobile Baby katika tuzo la kongamano la makampuni ya simu mwaka jana.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>