Ofisa Uhusiano wa Airtel TanzaniaJane Matinde akipiga penati kuashiria uzinduzi rasmi ya Airtel Rising Stars Mkoa wa Kinondoni.
Ofisa Uhusiana wa Airtel Tanzania akikagua timu kabla ya mechi kuanza.
Mchezaji chipukizi wa timu ya soka ya Sifa United ya Manzese Abuu Mohamed (kushoto) akichuana na mchezaji wa Makumbusho United Shabani Idd wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, Mkoa wa Kinondoni, iliyofanyika uwanja wa mpira wa shule ya msingi Mwanamanyala jijini Dar es Salaam Juni 23, 2013. Makumbusho United walishinda 3-1
Mchezaji wa timu ya soka ya Sifa United ya Manzese Yassin Saleh (kulia) akichuanana na Shaban Idd wa Makumbusho United wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya
Airtel Rising Stars, Mkoa wa Kinondoni, iliyofanyika uwanja wa mpira wa shule ya msingi Mwanamanyala jijini Dar es Salaam Juni 23, 2013. Makumbusho United walishinda 3-1
Mshambuliaji Ally Amin wa Makumbusho United (kulia) Abuu Mohamed wa Sifa United ya Manzese wakipambana vikali wakati wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, Mkoa wa Kinondoni, iliyofanyika uwanja wa mpira wa shule ya msingi Mwanamanyala jijini Dar es Salaam Juni 23, 2013. Makumbusho United walishinda 3-1
---
Timu ya Makumbusho United imeanza vema mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni baada ya kuibamiza timu ya Sifa United ya Manzese 3-1 katika mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa iliyopigwa kwenye uwanja wa Mwananyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Jumapili, Juni 23 2013.
Ilikuwa ni Sifa United walioanza kufunga goli katika dakika ya 16 wakati mchezaji wao hatari Jumbe Evon alipowatoka walinzi wa Makumbusho United na kuachia shuti kali iliyotinga wavuni moja kwa moja na kuibua hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo waliofika uwanjani kushuhudia mchezo huo. Goli hili lilidumu hadi mapumuziko.
Baada ya kupata maelekezo kutoka kwa kocha wao, wachezaji wa timu ya Makumbusho United walikianza kipindi cha pili kwa kasi kubwa na juhudi zao zilizaa matunda dakika tatu ndani ya kipindi cha pili wakati mchezaji mwenye kasi Willy Kalolo alipoipatia timu yake goli la kusawazisha.
Goli hilo la kusawazisha lilibadilisha kabisa sura ya mchezo huku vijana wa Manzese wakipambana kupata goli la kuongoza lakini walinzi wa Makumbusho walikuwa imara. Ilikuwa dakika ya 55 ambapo Makumbusho waliandika goli la pili kupitia kwa Ally Amin ambaye alipiga shuti kali na kuingia wavuni kabla ya Kalolo kufunga goli la tatu daikia ya 70 na kuzima ndoto za Sifa United za kushinda mechi hiyo
Michuano hiyo ya kusaka vipaji vya wanasoka chipukizi inaendelea kesho Jumatatu Juni 24 katika uwanja huo huo ambapo timu ya Mtakuja Beach itapambana na Sifa United.
Katika mkoa wa kisoka wa Ilala, Buguruni Youth Center (BYC) kesho Juni
24 watakuwa na kibarua kigumu watakapopambana na Bomubomu katika mechi
ya kukata utepe itakayofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Sekondari jijini Dar es Salaam. Kila upande umetamba kwamba utaibuka na ushindi.
Wakati michuano hii inaendelea, makocha watakuwa na kibarua kigumu cha kuchagua wachezaji ishirini bora kuunda timu za mikoa kwa ajili ya fainali za Taifa zitakazopigwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume
jijini Dar es Salaam kuanzia julai 2 2013.
Mkoa wa Temeke ambao ndio mabingwa watetezi wa ARS Taifa wanatarajia kuanza mashindano haya ngazi ya mkoa siku ya Jumanne Juine 25. Mikoa mingine inayoshiriki Airtel Airtel Rising Stars mwaka huu ni Morogoro, Mwanza, Mbeya, Tanga, Kigoma na Ruvuma.
Programu hii ya Airtel Rising Stars ni ya Afrika nzima likiwa na lengo la kuendeleza na kukuza mpira wa miguu katika bara la Afrika kwa vijana wanaochipukia waweze kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.
Fainali za ARS Taifa vile vile zitatumika kuchagua timu bora za wavulana na wasichana ambao wataiwakilishaTanzania katika mashindano ya kimataifa ambapo nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa mwezi ujao. Wachazeaji wengine watachaguliwa kwenda kwenye kliniki itakayoendeshwa na makocha kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United