Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Frontline, Lilian (kushoto) akiwa na Meneja Wateja Bi. Cecilia (kulia) wakiongea na wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali Tanzania waliohudhuria semina ya kuwajengea uwezo na kujua sehemu sahihi za kufanya kazi pindi wanapomaliza masomo yao iliyoandaliwa na British Council Tanzania kwa nia ya kuwakutanisha wanafunzi pamoja na makampuni na taasisi mbali mbali. Semina hiyo ilifanyika ndani ya Ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam.
Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Frontline, Lilian akiendelea kutoa somo kwa wanavyuo ambapo aliwakumbusha wavyuo hao kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa ya maisha yao.
Meneja Wateja Bi. Cecilia akitoa somo la kujitambua kwa wanavyuo waliotembelea meza ya kampuni hiyo, ambapo alisema ili uweze kufanya kazi kwa ufasaha ni vyema mtu kujitambua na kutambua majukumu yako.
Wageni mbali mbali nao walihudhuria.
Wanavyuo wakisikiliza kwa makini.
Somo limekolea.