Waziri mkuu Mizengo Pinda, akipokea mkataba wa mradi wa uhimarishaji wa Halmashauri za miji 18 uliozinduliwa leo, katika manispaa ya moshi, mkoani kilimanjaro, kuotka kwa mkurugenzi wa Benki ya Dunia, Philippe Donger, kulia ni waziri wa nchi Tamisemi, Hawa Ghasia.picha na Fadhili Athumani.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati), Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini, Philippe Donger kushoto) na waziri wa nchi Tamisemi, Hawa Ghasia(kulia) na baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 uliofadhiliwa na benki ya dunia katika picha ya pamoja jana, manispaa ya moshi mkoani kilimanjaro.picha na Fadhili athumani.
---
Fadhili Athumani, Moshi
WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Tanzania, Mizengo Peter Pinda amezindua mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 ya Dola milioni 225 inayofadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka benki ya dunia.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kuringe, Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Waziri Pinda amezitaka Halmashauri zote kuhakikisha zinajenga tabia ya kutenga Bajeti kwa ajili ya kutunza miradi yote inayoanzishwa hapa nchini ikiwemo Barabara na mradi huo.
Waziri Mkuu Pinda ameyasema hayo katika Warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri zote za miji 18 Tanzania Bara iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kuringe, manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, mradi uliofadhiliwa kutokana na Fedha za mkopo wa Dola milioni 225 kutoka benki ya dunia.
Pinda amesema endapo mradi huo unaolenga kuimarisha Halmashauri ya miji 18 Tanzania bara ya Iringa, Moshi, Tabora, Lindi, Babati, Kibaha, Geita, Mpanda, Bariadi, Sumbawanga, Shinyanga, Songea, Morogoro, Singida, Njombe, Musoma, Korogwe na Bukoba itasimamiwa vizuri na kutekelezwa kwa wakati itawezesha halmashauri kuibua vyanzo vingine vya mapato.
“Mheshimiwa Rais aliagiza na mimi narudia, Halmashauri zijenge tabia ya kutenga bajeti kwa ajili ya kutumnza miradi inayoanzishwa ikiwemo barabara na mradi huu tunaouzindua leo,” alisema Pinda.
Pinda amesema uzinduzi wa mradi huo ni thibitisho wa utayari wa Tanzania kutekeleza kazi kubwa na yenye kuleta matumaini ya maisha bora kwa wananchi wote na faraja kwa wageni watakaotembelea miji ya Tanzania siku zijazo.
Pinda ameishukuru Benki kuu ya dunia kwa kuiteua Tanzania kwa ajili ya mradi huo ambao utekelezaji barani aferika unaanzia nchini hapa kama mradi wa mfano huku akiwaagiza viongozi wote wa Halmashauri zote kumi na nane, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha mradi huo unafanikiwa .