Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma akitoa maelezo kwa mkuuu wa Wilaya ya Songea juu ya kikao chao cha ALAT ambacho wamejiwekea utaratibu wa kukutana kila baada ya miezi mitatu kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa ilani ya CCM.
Pia amewaagiza wajumbe wa ALAT mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri zao kuhakikisha wananchi wanatambua kuwa miradi iliyopo katika maeneo yao ni ya kwao na siyo ya Serikali.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akipongeza Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mkoa wa Ruvuma wakati wa ufunguzi wa kikao kwa utaratibu waliojiwekea wa kukutana kila baada ya miezi mitatu na kabla ya kufanya kikao kuanza kutembelea miradi kisha wanafanya kikao wakiwa na maelezo ama majibu sahihi ya kile wanachojadili kwa wakati huo.
Pia amewataka wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri kutumia fursa zilizopo katika kuwakwamua kiuchumi wananchi wa mkoa wa Ruvuma sio kutumia ofisi za halmashauri kwa ajili ya kujinufaisha wao wenyewe bali zitumike kwa manufaa ya wananchi na kuzitaka halmashauri zote Mkoani Ruvuma kuhakikisha zinakamilisha miradi yote ya utekelezaji kwa wakati badala ya kuleta visingizio kwamba imekwama kutokana na kukosa fedha kutoka Serikali kuu.
Toka kulia kwako ni Naibu Meya wa Manispaa ya Songea Wiloni Kapinga akiwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Songea mjini Gerad Mhenga wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mkoa wa Ruvuma
Makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT)mkoa wa Ruvuma Stevini Nana akimshukuru mkuu wa Wilaya ya Songea kuweza kuwa mgeni rasimi katika ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa Manispaa ukishirikisha wajumbe 25 toka wilaya za Mkoa wa Ruvuma.
Pia amewataka wajumbe kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa kwao na mkuu wa wilaya ya Songea wakati wa ufunguzi ambaye alihimiza zaidi uwajibikaji wa kila mmoja kwenye eneo lake.
Shukrani; http://demashonews.blogspot.com
Shukrani; http://demashonews.blogspot.com