Msanii wa ngoma za asili na Mkurugenzi wa bendi ya Mjomba Band Mrisho Mpoto akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni Mkwajuni wakati alipotangaza kuhusu kundi lake kuanza kampeni kubwa ya kuhamasisha wananchi kuhusu usafi wa mazingira mijini na vijijini kwa kunawa mikono na sabuni, kujenga na kutumia vyoo bora na kuboresha mzingira kwa ujumla ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia walengwa kwa kubadili tabia na njia mbadala za mawasiliano kuhusu elimu hiyo, Upatikanaji wa maji safi na salama na usafi wa mazingira bado ni tatizo kubwa kwa watanzania walio wengi, mwaka 2010 asilimia 9 tu ya wananchi waishio vijijini na asilimia 22 ya wananchi waishio mijini waliweza kupata huduma bora za usafi wa mazingira.
Kati ya sababu zingine, ni watu kutozingatia faida za usafi wa mazingira katika kampeni hiyo Mrisho Mpoto na kundi lake la mjomba Bendi wanashirikiana kwa pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, kushoto ni Mariam Mahamudu Afisa Afya, Mazingira Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii , Kampeni hiyo itaanza na mikoa ya Dodoma, Mara, Njombe, Rukwa na Tanga kabla ya kuendelea mikoa mingineMariam Mahamudu Afisa Afya, Mazingira Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii akizungumza katika mkutano huo kuzungumzia kuhusu kampeni hiyo, kulia ni Mrisho Mpoto Mkurugenzi wa Mjomba Band.Kundi zima la mjomba band likiwa katika mazoezi makali katika makao makuu ya kundi hilo Kinondoni Mkwajuni.Wakionyesha vitu vyao katika mazoezi hayoMrisho Mpoto akiimba katika mazoezi hayo ili kujiweka sawa kwa ajili ya kampeni hiyo kulia ni msanii wa kundi hilo anayejulikana kama Mbagala na katikati ni Mwimbaji wa kundi hilo Ismail.