Msanii Matonya amekamatiliwa kutokana na kufanya utapeli katika show aliyotakiwa kufanya katika ukumbi wa Jambolee uliyopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Baada ya kuja ukumbini akiwa amelewa hali iliyompelekea kushindwa kufanya show na kusababisha hasara katika ukumbi baada ya kufanya fujo ya kuvunja vitu ukumbi hapo, Ndipo waandaaji wa show hiyo walipoamua ifanyike kesho yake na kiingilo kiwe ni kununua bia .
Wakati huo msanii huyo alitakiwa akafanye show nyingine wilaya ya Mbinga ambayo ilikuwa ni sehemu ya mkataba wao lakini hakufanya hivo na matokeo yake akaamua kukata Tiketi kurudi Dar es Salaam, Baada ya kuvuja taarifa hizo walimfuata hadi alipokuwa amefikia ndipo walipokuta msanii huyo amehamia sehemu nyingine.
Hatua iliyochukuliwa ni kumvizia katika basi wakati wa asubuhi ndipo alipokamatwa, na kufikishwa katika mahakama ya mwanzo. Taarifa zaidi tutawaletea kesho mapema.
Shukrani demashonews blog kwa ushirikiano wako.