Na Ramadhani Issa, Serengeti.
Habari zilizotufikiableo majira ya jioni kuwa kuna ajali mbaya imetokea mbele kidogo ya NABI, Serengeti mbele ya golini kati ya basi la kampuni ya BUNDA EXPRESS na gari ya TOURs.
Akisimulia shuhuda wa ajali hiyo, Bw. Ramadhani Issa alisema kuwa "mimi na wenzangu wa nne tukiwa ni mashuhuda wa kwanza kuona ajali hiyo, Pia tukiwa ni watu wa kwanza kufika eneo la tukio na kuwatoa majeruhi.
Akisimulia shuhuda wa ajali hiyo, Bw. Ramadhani Issa alisema kuwa "mimi na wenzangu wa nne tukiwa ni mashuhuda wa kwanza kuona ajali hiyo, Pia tukiwa ni watu wa kwanza kufika eneo la tukio na kuwatoa majeruhi.
Nakumbuka muda mchache kabla ya ajali kutokea gari hiyo ya tours ilitupita kwa mwendo wa kasi kubwa mpaka hatukuweza kuona mbele zaidi kutokana na vumbi kubwa iliyokuwa ikivuma; hivyo ilitubidi sisi tupunguze mwendo ndipo tulipoona vumbi kubwa mbele yetu kumbe gari ile ya tours iliyotupita kwa mwendo wa kasi ilikuwa tayari imegonga basi kwa nyuma baada ya dereva wao kutaka kuover take kushindikana.
Wafanyakazi wanne wa Belila Loudge wameumia vibaya sana ila dereva wa gari hiyo ya tours hajaumia sana, sina budi kuwashukuru wazungu kutoka nje ya nchi kwa kusaidiana nao kutoa huduma ya kwanza kwasababu kama sio mchango wao majeruhi wote wangeweza kupoteza maisha palepale kwa sababu walivyokuwa wakitoka damu nyingi zaidi na ninahuzunika sana baada ya kuwasiliana na watu wa NGORONGORO getini kuwa wazembe kuchukuwa masaa matatu kufika eneo la tukio na kuwachukuwa majeruhi hao na kuwapeleka NDUTU waje kuchukuliwa na flay doctor kwa ajili ya kuwapeleka hospitali.
(Shukrani kubwa Ramadhani Issa kwa kuweza kutupatia taarifa hiyo ya ajali iliyotokea huko Serengeti).