Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

HATARI YA WATANZANIA KUPATA KATIBA AMBAYO HAITOKANI NA MAONI YAO: PROFESA LIPUMBA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu.

MWENYEKITI wa Chama cha wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kuwa kuna hatari ya Watanzania wakapata katiba ya nchi ambayo haitokani na maoni yao kwa mujibu wa sheria.

Kutokana na hali hiyo Profesa Lipumba, amemtaka Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba kutoharakisha mchakato huo hadi pale itakapopatikana rasimu ya Katiba kwa upande wa Tanzania bara.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaamj, leo Profesa Lipumba, alisema kuwa katika uchambuzi wa awali uliofanywa na chama chake umebaini upungufu kadhaa katika rasimu hiyo ya Katiba.

Alisema katika mapendekezo yake ya msingi ni kwamba kura ya maoni isubiri kukamilishwa kwa rasimu ya katiba ya Tanzania Bara na pindi zikijadiliwa zijadiliwe kwa pamoja na wananchi.

“Wananchi wamechoka wanataka mabadiliko na katika hili ni lazima iandaliwe pia na rasimu ya Katiba kwa upande wa nchi ya Tanzania Bara ili ziweze kujadiliwa zote kwa pamoja na kupigia kuwa ya maoni na Watanzania wote,” alisema Profesa Lipumba.

Akizungumzia ibara ya 181 (4), ya rasimu hiyo ya Katiba Profesa Lipumba, alipinga hatua ya kumpendekeza watu wanaotakiwa kuomba kazi hiyo ni lazima wawe ni majaji wa Mahakama Kuu.

“Jambo hili halikubaliki hata kidogo eti wanaotakiwa kuomba kazi ya uenyekiti ni lazima wawe majaji wa Mahakama Kuu, kwani kazi hii ni vema iwe inaombwa na mtu yeyote mwenye sifa na tukiondoe kigezo hiki.

“Kwa muda wa miaka 15 Tume ilikuwa inaongozwa na Jaji mstaafu Lewis Makame, lakini bado ilikuwa ni bomu kwa watanzania na vyama vya upinzania hasa inapofika wakati wakudai haki za msingi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>