Wakati msafara wa msiba wa marehemu Albert Mangwer ambaye ni mtoto wa kumi wa familia hiyo, mama yake mzazi hali yake si nzuri kutokana na mshtuko alioupata tokea kusikia kifo cha mwanae hali yake imekuwa si ya kuridhisha maana alikuwa amelazwa hospitalini na sasa ametoka ila bado afya haijatenge,aa kuokana na kupadwa kwa presha. Mama yake mangwer alizimia siku ya kwanza kupewa msiba na baadae alizinduka nakupata ahueni ila alizimia tena mara ya pili. Mwili wa mwanae Albert Mangwer umeliwasili jana kutoka Afrika Kusini na kuagwa leo jumatano viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam na umesafirishwa leo kwenda mjini Morogoro kwa ajili ya maziko yatakayofanyika kesho Alhamis.
↧