Tigo Tanzania leo imezindua huduma mpya ya malipo ya biashara kupitia simu ya mkononi ambayo itawawezesha wateja wake kununua bidhaa mbalimbali kupitia Tigo Pesa.
“Tigo inafanya jitihada za juu kabisa kuhakikisha inavumbua bidhaa na huduma zinazoongeza thamani na kurahisisha maisha ya watanzania kwa ujumla. Dhamira yetu ya kuwapatia watanzania huduma mbalimbali zinazokidhi mahitaji yao kupitia simu za mkononi ndio kitu kinachotusukuma sisi kama kampuni ya simu iliyobobea kwenye ubunifu. Kupitia huduma hii ya malipo ya biashara ya simu za mkononi Tigo inapanua uwigo wa Tigo Pesa na kuifanya kuwa ni zaidi ya kutuma na kupokea pesa tu, kwa kuwawezesha wateja wetu kuwa na mfuko wa kidijitali wa kuhifadhi pesa ambao unaweza kutumika kununua na kuuza bidhaa. Huu ni ubunifu mkubwa sana kwa upande wetu!” Alisema Bwana William Mpinga, meneja wa chapa ya Tigo.
Bwana Mpinga aliendelea kufafanua kuwa “Kutumia malipo ya biashara ya simu za mkononi ni njia nyepesi na ya usalama kabisa ya kufanya biashara. Hatari zinazoendana na kubeba fedha zitapunguzwa kwa kiasi kikubwa sana sababu wateja watakuwa wanalipia bidhaa kwa kutuma Tigo Pesa. Hata Bishara zitapunguziwa hatari ya wizi wa fedha kwani mauzo yao ya siku yatakusanywa na kupelekwa moja kwa moja kwenye mfuko wao wa Tigo Pesa ambapo wanaweza kutuma fedha zao kwenye akaunti zao za benki kwa zile benki zizazoshirikiana na Tigo Pesa. Vile vile, huduma hii itafungua milango kwa biashara nyingi zinazohusiana na machukuzi hivyo kuwapatia watanzania mbinu mbadala za ajira. Kwa mara nyingine tena tunawajenga wateja wetu muhimu kupitia Tigo Pesa kwa namna ambayo haijawahi kufanyika, na hii ndio dhamira kuu ya chapa ya Tigo!”
Zaidi ya wafanyabiara wa Tigo Pesa elf hamsini nchi zima wameshajiunga kwenye huduma hii. Namba hii inatarajiwa kukua kadri siku zinavyoendelea hivyo kuwapatia watanzania huduma bora za kufanya biashara.