Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19676

RAIS KIKWETE AKABIDHI VITABU 201 KWA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI, AAGANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA NA RWANDA

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi baadhi ya vitabu   na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange. Rais Kikwete amekabidhi vitabu hivyo 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa January 9, 2015. Rais kikwete, ambaye ameshachangia jumla ya vitabu 2752 katika maktaba ya chuo hicho na chuo cha Monduli katika vipindi tofati, amesema elimu imo vitabuni, na ili kuelemika yapaswa mtu asome vitabu, na kwamba taasisi ya elimu inakamilika ikiwa na vitabu.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange alipokuwa akimshukuru kwa kutoa vitabu 2752 kwa Chuo cha Ulinzi na makataba zingine za JWTZ wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa January 9, 2015.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na maafisa waandamizi wa JWTZ wakiangalia vitabu wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa January 9, 2015.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19676

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>