Wanafunzi wa Madrasa Shathil ya Chang’ombe jijini Dar es Salaam wakisoma Qaswida wakati wa sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W.) zilizofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Zakia Bilali (katikati) akiwa na Wake wa makamo wa Pili wa rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (kushoto) na Mama Pili balozi Seif (kulia) pamoja na Wake wa Viongozi mbali mbali na wananchi wa kawaida wakijumuika katika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad S.A.W yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja ambapo hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguosita. (Picha na Ikulu, Zanzibar)
Ustadh salum Rashid kutoka Amani Wilaya ya Mjini Unguja akisoma Mlango wa Barzanji(4) wakati wa sherehe za Maulid Matukufu ya kuzaliwa bwana Mtume Muhammad (S.A.W.) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein.
Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein.
Akina Mama kutoka mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja na Vitongoji vyake wakiwa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja palipofanyika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad S.A.W ambapo hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguosita na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (katikati) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif,Kadhi Mkuu wa zanzibar Sheikh Khamis Haji (kulia) Waziri wa katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary akifuataiwa na makamo wa Pili wa Rais Alhaj Seif Ali Iddi wakisimaa kwa pamoja na waislamu wengine na Viongozi wakati wa Kumswalia Bwana Mtume Muhammad S.A.W.katika sherehe ya Maulid iliyofanyika jana
viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja.
viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja.
Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa katika maandamano ya sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Madrasatul Dhuriyatul Islamia kutoka Kisiwani Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja wakisoma Qaswida wakati wa sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein. (Picha na Ikulu, Zanzibar)