1) Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kulia mbele) na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani (wa tatu kushoto mbele), wakiwaongoza wafanyakazi wa Airtel Tanzania na wanafunzi kwenye matembezi ya hisani yenye lengo la kuchangisha pesa kiasi cha shilingi milioni 10, kwa ajili ya kuendelea kuboresha Shule ya Msingi Kumbukumbu , yaliyoanzia katika Makao Makuu ya Airtel , Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kupitia Bongoyo, Haile Selasie na kuishia shuleni hapo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
3) Wafanyakazi wa Tanzania na wanafunzi wakiwa kwenye matembezi ya hisani yenye lengo la kuchangisha pesa kiasi cha shilingi milioni 10, kwa ajili ya kuendelea kuboresha Shule ya Msingi Kumbukumbu , yaliyoanzia katika Makao Makuu ya Airtel, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kupitia Bongoyo, Haile Selasie na kuishia shuleni hapo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
4) Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani, funguo za kisima kipya cha maji safi kilichojengwa kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi wake, katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Malya (kushoto), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa tatu kushoto), na Mwenyekiti wa Shule hiyo, Mwemba Mwilima.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani (kulia) akifungua ili kukagua kisima kipya cha maji safi kilichojengwa kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi wake, katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto), wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Malya (kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa tatu kushoto).
Na Mwandishi Wetu.
Kampuni ya Airtel leo imeendesha matembezi ya hisani ili kuchangisha pesa kwajili ya kuendelea kuboresha shule ya msingi kumbukumbu iliyopo jijini Dar es salaam
Matembezi yenye lengo la kupata pesa ili kufanya ukarabati wa darasa la watoto na kununua viti na meza za kukalia yameetimishwa kwa uzinduzi wa kisima cha maji kilichojengwa kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na wafanyakazi wake ili kukabiliana na tatizo la maji shule hapo
Akiongea wakati wa kuzindua kisima hicho mgeni rasmi , Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia na watoto Mh. Sophia Simba alisema” naunga mkono juhudi zilizofanywa na Airtel katika kuendelea kuboresha mazingara ya utoaji elimu shuleni hapa. Nimefurai kuona kuwa Airtel haikuridhika na ujenzi wa kisima hii tu bali wameamua kuchua hatua nyingine ya kushirikisha wadau mbalimbali katika kutatua changamoto walizoziona shuleni hapa.
Leo tumetembe kwa pamoja ili kuweza kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 10 zikazowesha kazi ya kuendelea kuboresha mazingara ya shule hii kuendelea.
Serikali inaunga mkono dhamira hii na jitihada hizi zinazoenda sambamba na kauli mbili yetu ya Matokeo makubwa sasa na kuhakikisha tunaboresha maeneo muhimu hususani elimu kwani vijana hao ndio nguvukazi na taifa la kesho. Natoa wito kwa mashirika mengine watu binafsi na taasisi mbalimbali kujitokeza na kuchangia katika shughuli za jamii ili kukubiliana na changamoto tulizo nazo sasa.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema” nawashukuru wafanyakazi wa Airtel na kila moja aliyeshiriki hapa kwa kujitoa katika kusaidia jamii, sisi Airtel tumejipanga kutimiza dhamira yetu ya kuchangia katika kuhakiksha tunachangia katika sekta ya elimu kwa kuendelea kutoa vitabu na kuboresha mazingira ya shule. Kupitia mradi wa Airtel Shule yetu tumeweza kuzifika shule nyingi kwa kuwapatia nyenzo muhimu katika elimu na leo tumewafikia shule ya msingi kumbukumbu tukiwa na lengo na kuendelea kuboresha sekta ya elimu.
Mpango huu wa Airtel Tunakujali ni endelevu bado tutakuwa shughuli nyingi zaidi na shule nyingi zikipokea misaada hivyo tunawaomba wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana nasi.
Kwa upande wake mfanyakazi wa Airtel Bi Veneranda Boniface Alisema amejisikia furaha kutumia jumamosi yake kutembea kwaajili yakusaidia jamii, hii ni sehemu pia ya mazoezi lakini zaidi ni njia pekee ya kuniwezesha mimi kwa nafasi yangu katika jamii kushiriki kuchangia.
Matembezi hayo ya hisani yalianzia katika makao makuu ya Airtel yaliyoko Moroco Dar esaalam na kwenda njia ya Alihasan Mwinyi, kupitia Kaunda, Bongoyo , haileselaile , Ali hassani Mwinyi na kuishia katika shule ya msingi Kumbukumbu.