MAANA PESA NDIYO ILIFANYA TUSIWE NA TANGA NDUGU
PESA ILILETA UBAGUZI KATI YA LOYOLA NA PUGU
PESA NDIYO ILICHOCHEA BEEF YA NICE NA DUDU
NA PESA NDIYO ILIMALIZA VITA YA RUGE NA SUGU!!!
Maana yake:-
Unapozungumzia pesa basi kila mtu atakuja na tafsiri yake na mifano na matukio yake yaliyosababishwa na pesa.Ni kitu chenye maana pana sana na ni kitu kilichokaa nyuma ya vitu vingi vilivyowahi kutokea. Pengine bila pesa visingetokea.
Familia nyingi zinakutana na matatizo mengi sana hasa pale msiba unapotokea, hususani wa ile nguzo ya familia. Hali hii hupelekea hata msiba unaisha na ndugu wanashindwa kukutana na kupanga lolote na hata kulala matanga hawalali, wanatawanyika. Utasikia wakisema "Tumeshamzika tukafanye yetu sasa",... tukilala matanga ni gharama zingine tena.
Kuna utofauti mkubwa sana kati ya mwanafunzi wa shule ya Loyola na Pugu hili lipo uchi kabisa. Utofauti huu huleta ubaguzi katika baaadhi ya vipaumbele.
Nilipita kwenye familia ambayo ina mtoto wa Pugu na hapo hapo yupo wa Loyola. Baba na mama yao ni mmoja lakini kuna utofauti wa malezi ya kielimu na vitu vingi baina ya watoto hawa wawili... unadhani kwanini?
Pesa ilichochea ugomvi wa Mr. Nice na Dudu.....unadhani Mr. Nice bila zile pesa ule ugomvi ungekuwa kubwa kiasi kile?
Hapa sasa "Pesa ilimaliza vita ya Ruge na Sugu"!!
-Kiufupi ni kuwa issue ya kaka Sugu kuingia katika vita hii kama ilivyosemwa awali na ilivyoonekana POINT ilikuwa kuitetea sanaa, ambayo ni wasanii pia wakiwemo ndani hapo... kuwa wanachokipata hakistahili kulinganisha na kazi wanayofanya!! malipo mabovu ya show, uuzwaji mbovu wa kazi za sanaa unawafaidisha wengine kuliko wasanii, na mengine mengi sana tuliyasikia!! ambayo kimsingi yote yanaegemea kwenye kipato = Pesa.
Lakini baadae ikaja semwa na pande zote mbili zikakiri kuwa songombingo hilo limeisha baada ya pande zote mbili kukubaliana kuwa yote yaliyokuwa yakilalamikiwa yameeleweka na upande wa kaka Ruge umekubali kuyamaliza yote yaliyokuwa yakilalamikiwa kuwa sasa yameisha na yanatekelezwa.
Sasa hiyo itufundisha nini? kama yameisha ina maana tatizo la malipo duni ya wasanii, tatizo la wasanii kuingiza pesa nyingi na kulipwa kidogo tofauti na wanachoingiza na yote yaliyoongelewa SASA YAMEFIKIA KIKOMO. BASI NI HABARI NJEMA KWA WASANII.
Na hiyo yote ni nini?
- Ni kuwa sasa watapata kipato sawa na haki yao.
-Wataifanya sanaa yao kwa njia sahihi na za faida kama ilivyokuwa ikihitajika katika vita hiyo.
-Na wataiona faida ya sanaa kwa ujumla.
KIPATO=MALIPO=PESA
BASI PESA NDIYO IMEMALIZA VITA YA RUGE NA SUGU.
2030 YA R.O.M.A
NAYAJIBU NINAYOULIZWA NA YANAYOHITAJI UFAFANUZI.